Je nawezaje kula vyema kwa gharama ndogo

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Ikiwa pesa hazitoshi, ni vyema kuzitumia vyema. Hapa kuna pendekezo kwa kupata vitamini, madini na protini kwa bei nafuu.

Vyakula vya Protini: Maharagwe, mbaazi, ndengu na vyakula vingine aina hiyo ni vizuri, na bei yake ni nafuu. Unaweza kulowesha vyakula hivi hadi wakati vikianza kumea, kisha pika, kwani ndio vina wingi wa vitamini. Mayai pia ni ya bei nafuu na yana wingi wa protini. Mara nyingi, maini, moyo, figo, damu na samaki huuzwa kwa bei nafu kuliko aina zingine za nyama, na ni lishe bora.

Nafaka Mchele, ngano na aina zingine za nafaka ni lishe bora ikiwa ngozi yao haitolewi wakati wa kusyaga.

Mboga na Matunda Ni bora ule mboga na matunda baada ya kuyavuna. Hakikisha kuwa unayahifadhi mahali pakavu ili kutunza vitamini zake. Pia mboga kwa kutumia maji kidogo, kwa sababu vitamini kutoka kwenye mboga huenda kwenye maji wakati wa kupika. Kisha, tumia maji haya kwa kutengenezea supu na uinywe.

Maganda ya baadhi ya mboga kama vile karati au cauliflower yana wingi wa vitamini na yanaweza kutumika kuengeneza supu. Kwa mfano, matawi ya mhogo yana hadi mara 7 ya protini na vitamini zaidi ya mizizi yake. Baadhi ya matunda yanayomea bila kupandwa yana wingi wa vitamini C na sukari asilia na vitamini.

Ikiwa una mahali padogo, itakuwa vyema ukipanda mboga zako ambazo zitakupatia lishe bora kwa bei nafuu.

Vyakula vya maziwa Ni lazima vyakula hivi viwekwe mahali palipo baridi na penye giza. Vyakula hivi husaidia kujenga mwili kwa protini na calcium.

Epuka kununua vyakula vilvyotengenezwa. Ikiwa wazazi watatumia pesa walizoweka kwa matumizi ya peremende au kinywaji kama soda na kutumia pesa hizo kwa kununua lishe bora, basi watoto wao watakuwa na afya bora. Kwa sababu watu wengi wanaweza kupata vitamin wanazohitaji kutoka kwa chakula, ni vyema kutumia pesa kwa kununua lishe bora bila kutumia pesa hizo kwa dawa au sindano. Ikiwa ni lazima utumie vitamins, meza dawa. Hufanya kazi kama kudungwa sindano, ni salama na bei nafuu.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010412