Watoto wanaweza kujeruhiwa wakati wanavuka barabara au wakiwa tu wanatembea barabarani au wanapocheza barabarani. Watoto wadogo huwa hawafikirii kabla ya kwenda barabarani.
Ni wajibu wa familia kuhakikisha kuwa:
wanawaangalia watoto kwa umakini
wanaweka ua kuzunguka nyumba, kufunga lango kuu ili kuzuia watoto wadogo kwenda barabarani
wafundishe watoto wadogo kuwa wasivuke barabara, wala kutembea barabarani isipokuwa wakiwa wameambatana na mtu mzima au mtoto aliyewashinda kwa umri
watoto hawachezi karibu na barabara
wafundishe watoto kuwa wasikimbilie mipira au vifaa vya kuchezea ambavyo huenda karibu na barabara
wafundishe watoto kutembea kando kando ya barabara, wakielekea kule ambako magari yanatoka
ikiwa kuna njia kando ya barabara, wafundishe watoto kuitumia badala ya kutembea barabarani