Je nawezaje kuzuia kiungulia au chakula kukosa kusagika

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kiungulia husababisha hisia kama kuchomeka kwenye koo au kifua. NI kawaida kuwa na hisia hii baada ya kula au ukiwa umelala chini, na huja pale uja uzito unapokaribia mwisho wake.

Jinsi ya kuzuia:

  • Kula mara nyingi kwa siku badala ya mara moja.
  • Usile vyakula vyenye pilipili au mafuta mengi.
  • Kunywa maji kwa wingi.
  • Usilale chini baada ya kula.
  • Unapolala, hakikisha kichwa chako hakijalingana na tumbo lako.
  • kunywa maziwa au bicarbonate kidogo na maji, au dawa ya kupunguza kiungulia.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010709