Kabla ya kutayarisha chakula, kula na kabla ya kuwalisha watoto, osha mikono yako kwa maji na sabuni. Kuosha mikono huzuia kusambaa kwa magonjwa. Hakikisha kuwa una kitambaa maalum cha kukausha mikono. Hakikisha kuwa unakiosha kila mara na kukianika kwenye jua ili kikauke. Unaweza kuikausha mikono yako kwa kuitingisha hewani.
Osha au toa maganda kwenye mboga na matunda ambayo huliwa yakiwa mabichi.
Hakikisha kuwa nyama mbichi, kuku au samaki haigusi vyakula vingine ambavyo huliwa vikiwa vibichi. Osha mikono yako, kisu na ubao wa kukatia vyakula hivi unapomaliza kukata nyama.
Usikohoe, wala kutema mate, wala kutafuna perememnde karibu na chakula ii mate yako yasiingie kwenye chakula.
Usiwaruhusi wanyama kulamba vyombo. Ikiwezekana, hakikisha kuwa wanyama hawaingii jikoni.
Tupa chakula mara kinapoharibika.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.