Je nawezaje kuzuia malaria wakati wa uja uzito

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Malaria ni ugonjwa hatari sana kwa akina mama waja wazito. Kama njia ya kuzuia maambukizi, haswa kwa akina mama wanaoishi maeneo yanayojulikana kwa malaria, na haswa akina mama ambao ni waja wazito kwa mara ya kwanza, na ambao mara nyingi hawataonyesha ishara ya kuugua, ni muhimu sana wameza dawa za kuzuia malaria katika miezi mitatu, ya pili na ya tatu. Vile mhudumu wa afya aliyehitimu atakavyokushauri. Mhudumu wa afya anafahamu ni dawa zipi za malaria zinafaa. Ni muhimu pia kwa mama mja mzito kulala kwenye neti au wavu iliyotibiwa kwa dawa za kuzuia mbu.

Lazima wanawake waja wazito ambao wana ishara za kuambukizwa viini vya malaria watibiwe mara moja na mhudumu wa afya aliyehitimu kwa kutumia dawa aina ya 'quinine' katika miezi mitatu ya kwanza, na ACT katika miezi mitatu ya pili na ya tatu.


Sources