Je nawezaje kuzuia saratani

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Haijulikani kwa uhakika nini husababisha saratani.

Kuwa na afya njema kunaweza kuzuia saratani aina nyingi. Hii inamaanisha kula vyakula vya afya na kuepuka vitu ambavyo husababisha saratani. Kwa mfano:

Usivute wala kutafuna tumbaku.

Jaribu kuepuka kemikali hatari nyumbani mwako au kazini, ikiwemo vyakula ambavyo vimekuzwa na kuhifadhiwa na kemikali.

Uvimbe kwenye matiti ni jambo la kawaida kwa wanawake, haswa uvimbe laini, uliojaa maji (huitwa cysts). Uvimbe huu hubadilika mara kadhaa katika siku zake za mwezi, na wakati mwingine huwa chungu zinapoguzwa. Uvimbe mchache kwenye matiti ya wanawake husababisha saratani. Lakini kwa vile kuna uwezekano wa saratani ya matiti, ni vyema mwanamke akague matiti yake kila mwezi.

Saratani ya maini inaweza kusababishwa na hepatitis B na C. Hepatitis B na C inaweza kuzuiwa kwa kushiriki ngono salama na kutoshirikiana sindano. Hata chanzo dhidi ya hepatitis B. Watoto wachanga pia wanaweza kupewa chanjo baada ya kuzaliwa. Watu wazima wanaweza kupewa chanjo wakati wowote.

Chanjo mpya kwa jina "HPV", ya kulinda vijana kutokana na saratani ya njia ya uzazi imevumbuliwa na inatumika katika mataifa mengi. Lazima wasichana wachanjwe kabla hawajaanza kushiriki ngono. Muulize mhudumu wa afya kama inawezekana pale unaishi.

MUHIMU: Saratani inaweza kutibiwaikiwa itagunduliwa mapema. Inapogunduliwa mapema, maisha ya mwanamke yanaweza kuokolewa, kwa sababu atapata matibabu haraka, kabla saratani haijasambaa. Nenda kwa uchunguzi wa saratani katika kituo cha afya kilicho karibu na wewe.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011404