Je nawezaje kuzuia shida za kiafya zinazotokana na moshi
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Ili kupunguza hewa yenye moshi unayopumua:
Pikia mahali ambapo kuna hewa ya kutosha. Ikiwa huwezi kupikia nje, hakikisha kuwa kuna amadirisha mawili kwenye chumba hicho. Hii huleta hewa safi, ili moshi uondoke.
Mnaweza kupika kwa zamu na wanawake wengine. Hivi, kila mwanamke atapumua moshi kidogo.
Tafuta njia mbadala za kutayarisha chakula ambazo hucukua muda mfupi (lakini chakula kinaiva). Hivi, utapumua moshi kidogo, na utatumia kuni chache.
Chakula hupikika haraka ikiwa:
Tumia jiko ambazo hutoa moshi kidogo. Hii ni njia nzuri ya kuzuia shida za kiafya ambazo husababishwa na moshi unapopika. Jiko ambazo hutumia kuni chache hutoa moshi kidogo na zinapatikana katika maeneo unamoishi, lakini zinaweza kutengenezwa na vifaa vya kiasili.