Je nawezaje kuzuia ugonjwa wa malaria kwa ujumla
Malaria husambazwa kutokana na kuumwa na mbu, kulala chini ya neti ambayo imetibiwa ni njia bora ya kuzuia kuumwa na mbu.
Watu wote katika jamii wanafaa kukingwa dhidi ya kuumwa na mbu haswa watoto na wanawake wajawazito. Kinga inahitajika baada ya jua kutua na kabla ya jua kuchomoza, wakati mbu wanaosambaza malaria anapouma.
Neti au wavu zilizotibiwa hukaa muda wa miaka mitatu na haihitaji kutibiwa tena. Neti au wavu hizi zilizotibiwa hupeeanwa na kampuni zinazotoa huduma za kuzuia malaria na zaweza kupatikana katika vituo vya afya. Neti hizi hupeanwa bila malipo haswa kwa wanawake wajawazito na watoto. Pia, neti aina hii inaweza kupatikana kwa soko au wakati wa huduma za kuwaelimisha wanawake kuhusu malaria mijini. Katika visa vichache ambapo neti ambazo hazijatibiwa zinapotumika, wahumu wa afya waliohitimu wanaweza kupeana ushauri unaofaa jinsi ya kutibu neti hizo.
Neti zilizotibiwa zinastahili kutumiwa kwa mwaka wote, hata kama kuna mbu wachache, haswa wakati wa ukame.
Nchi zingine hutoa huduma za kupuliza kuta za nyumba na dawa ya kuuwa mbu. Jamii zastahili kujumuika na wanaopuliza kuta na dawa hiyo ili kuhakikisha nyumba zote zimepulizwa dawa hiyo.
Kando na kutumia neti zilizotibiwa, au kama neti zizlizotibiwa hazipatikani au kutumiwa, njia zingine mbadala zinaweza kusaidia, lakini si bora sana kuliko neti zilizotibiwa. Njia hizo ni: