Ikiwa viini vya malaria au minyoo inasababisha upungufu wa damu mwilini, hakikisha unatibu malaria kwanza.
Kula vyakula vyenye wingi wa maidini aina iron pamoja na vyakula vyenye vitamini A na C, ambavyo husaidia mwili kufyonza iron. Matunda na nyanya zina wingi wa vitamini C. Maboga yenye rangi ya kijani au njano pia yana wingi wa vitamini A. Ikiwa mwanamke hatakula vyakula vya kutosha vilivyo na wingi wa madini aina iron, atalazimika kumeza tembe za kuongeza damu.
Usinywe chai ya rangi au kahawa, au kula maganda ya nafaka wakati wa makuli. Hivi vinaweza kuzuia mwili wako kufyonza madini aina iron kutoka kwenye vyakula.
Kunywa maji safi ili kuzuia maambukizi kutokana na viini.
Tumia choo cha kuchimba kwa kwenda haja kubwa, na kuzuia mayai ya minyoo kusambazwa kwenye chakula na vyanzo vya maji. Ikiwa kuna shida ya minyoo unakoishi, hakikisha unavaa viatu.
Pata watoto walioachan kwa muda wa miaka miwili. Hii itaupatia mwili wako nafasi ya kujiwekea madini aina ya iron kabla hujashika mimba tena.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.