Je ni vipi ambavyo ninaweza kutupa takataka kwa njia inayofaa

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Ikiwa hakuna mfumo mwafaka wa uzoaji taka katika jamii, kila familia inapaswa kuwa na shimo la taka ambapo takataka za pale nyumbani zitazikwa au kuchomwa kila siku.

Ikiwezekana, zika au choma takataka au tengeneza mbolea. Ikiwa utazika takataka, hakikisha kuwa shimo lina kina kirefu ili kuzuia uvamizi wa wanyama na wadudu.

Ikiwa takataka haijazikwa, jenga ua kulizingira shimo lile na ufunike takataka kwa kutumia udongo ili kupunguza nzi.

Tumia mabaki ya chakula kama mbolea kwa mimea yako.

Tafuta njia mwafaka za kuondoa vifaa hatari na vyenye sumu. Kwa mfano, usichome plastiki, kwa sababu mvuke wake ni sumu, hasa kwa watoto, wazee na watu wanaougua.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010109