Je ni vipi ambavyo usafi unaweza kuzuia kusambaa kwa viini vya magonjwa
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Usafi katika jamii (haswa ikizingatiwa kuwa na vyoo safi), usafi pale nyumbani, usafi wa mtu binafsi, yote ni muhimu ili kuzuia magonjwa kwa kuzuia kusambaa kwa viini vya magonjwa.
Kwa mfano:
Baadaye, mtoto yule hulia, kisha mamake ambembeleze na kusafisha vidole vyake kwa kuvipangusa akitumia nguo yake. Kinyesi kile kinajipaka kwenye mikono ya mama.
Kwa vile mama yule ana shughuli nyingi ya kuitayarishia familia yake chakula, anasahau kuosha mikono yake kabla ya kuanza kupika. Anatumia nguo yake kushikilia sufuria ili asichomoke mikono, huku akisahau kuwa nguo hiyo sio safi.