Je ni vipi ninaweza kuimarisha uhusiano wa kingono katika miaka ya uzeeni

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kwa baadhi ya wanawake, kukomaa kwa hedhi humaanisha mwisho wa shughuli za ngono katika ndoa. Akina mama wengine huwa na hamu sana ya ngono kwa sababu hawana hofu ya kushika mimba. Hata hivyo, wanawake wote wanahitaji upendo. Hakuna ushuhuda wa kuonyesha kuwa, kwa sababu ya umri, mwanamke hawezi kufurahia ngono.

Baadhi ya mabadiliko katika mwili wa mwanamke humzuia kushiriki ngono:

  • Huenda hana hamu tena ya kushiriki ngono (wanaume pia huathirika).
  • Sehemu yake ya uzazi hukauka, na hii hufanya tendo la ngono kutofurahisha, au kumfanya mwanamke akapata maambukizi kwenye sehemu hii au katika njia ya kupitisha mkojo, kwa urahisi. Hii pia huongeza hatari ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI.

Je, naweza kufanya nini kupunguza shida hizi?

Tenga muda zaidi kabla ya kushiriki ngono, ili sehemu yako ya uzazi iweze kujitengenezea unyevunyevu wake. PIa unaweza kutumia mate, mafuta yaliyotengenezwa kutokana na maboga kama vile (zaituni na mahindi - corn oil na live oil), au mafuta mengine kama vile K-Y jelly, wakati wa ngono. Usitumie mafuta yalitotengenezwa kwa petroli au mafuta yenye marashi ilikuongeza unyevunyevu kwenye sehemu ya uzazi. Hii husababisha mwasho.

JAMBO MUHIMU: Ikiwa unatumia mipira, usitumie mafuta kuleta unyevunyevu. Mafuta huharibu mipira na inaweza kupasuka.

Ikiwa mwenzako atashindwa kushiriki ngono kwa sababu hayuko tayari, kuwa na subira. Unaweza kumpapasa kidogo.

Usijaribu kufanya sehemu yako ya siri kuwa kavu kabla ya kushiriki ngono. Ili kuzuia kusumbuliwa na mkojo, hakikisha kuwa unaenda haja ndogo baada ya kushiriki ngono ili kuondoa viini.



Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010910