Je ni vipi nitahakikisha ninapata Vitamini A ya kutosha
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Vitamini A husaidia kuzuia upofu wa usiku na pia huzuia maambukizi fulani. Wanawake wengi waja wazito wana shida za kuona wakati wa usiku, jambo ambalo linamaanisha kuwa huenda lishe lao halikuwa na viatamini A kabla ya wao kushika mimba. Shida hii huonekana mimba inapoendelea kukua.
Ukosefu wa vitamini A pia husababisha upofu katika watoto. Kwa kula vyakula vilivyo na wingi wa vitamini A wakati wa uja uzito, mwanamke anaweza kuongeza viwango vya vitamini A kwa mtoto wake kupitia kwa maziwa yaek.
Ni vyema mwanamke ale maboga yenye rangi ya kijani, na matunda yenye rangi ya machungwa, yaliyo na wingi wa vitamini A.