Je nifanyeje ikiwa hedhi yangu itakuja haraka au kutokwa damu nyakati zingine

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Huenda kuna tatizo fulani ikiwa hedhi zako zinakuja kabla ya wiki tatu au kuisha au kuja mara kwa mara bila mpango.

Vyanzo vinavyokisiwa:

  • Huenda ovari haikutoa yai.
  • Kuna uwezekano kuwa una 'fibroids', 'polyps' au saratani tumboni, hasa ikiwa hedhi zako ni nzito na haziji kwa wakati wake.
  • Kumeza dawa ya 'estrogen' baada ya kukomaa kwa hedhi.
  • Mbinu fulani za upangaji uzazi - kama vile tembe na sindano - hukufanya uvuje damu kila mara.
Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010223