Je nifanyeje ikiwa nitavuja damu kupita kiasi au hedhi yangu ikitoka kwa muda mrefu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

  • hedhi huwa nzito ikiwa sodo au kitambaa unachotumia kitalowa katika muda wa lisaa limoja.
  • hedhi pia ni ndefu ikiwa itaendelea kwa muda wa zaidi ya siku nane.
  • hedhi ikitoka na kufanana kama vipande vidogo vya maini, hii ni ishara ya hedhi nzito.
  • hedhi inayoendelea kwa wiki kadhaa, miezi au miaka husababisha shida ya upungufu wa damu mwilini.

Sababu zinazokisiwa.

  • Huenda homoni haziko sawa kwa hivyo ovari haitoi yai. Hii ni kawaida kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20 na wanawake wa umri zaidi ya 40.
  • Huenda mbinu ya kupanga uzazi iliyotiwa tumboni inasababisha hedhi nzito.
  • Kuharibika kwa mimba, hata kama hukujua kuwa wewe ni mja mzito.
  • Ikiwa una maumivu tumboni pamoja na kuvuja damu, huenda umeshika mimba na haiko mahali inastahili kuwa kwenye mshipa tumboni. TAHADHARI. Nenda hospitalini mara moja.
  • Huenda pia una shida ya mshipa wa tezi.
  • Huenda una shida ya mojawapo ya 'fibroids' au 'polyps' au saratani tumboni.

TAHADHARI: Ikiwa hedhi yako ni nzito, muone mhudumu wa afya ambaye amepata mafunzo ya jinsi ya kukagua sehemu za uzazi, na ikiwa:

  • damu inavuja sana kutoka sehemu yako ya uzazi. .
  • hedhi yako imekuwa nzito na kukaa kwa muda, katika kipindi cha miezi 3.
  • unafikiri kuwa wewe ni mja mzito.
  • unapata maumivu makali pamoja na hedhi yako.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010221