Je ninawezaje kujenga choo cha shimo
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Chimba shimo la upana wa Nusu Mita, urefu wa Mita Moja Unusu, na kina cha Mita Tatu.
Funika choo, huku ukiacha shimo la mraba wa sentimita 20 kwa sentimita 30.
Tumia vifaa vya kawaida kwa kutengeneza kuta na paa.
Hakikisha kuwa, choo kiko umbali wa mita 20 kutoka kwa nyumba zote, mabwawa ya maji, chemichemi au mito. Ikiwa lazima iwe karibu na mahali ambapo watu huteka maji, hakikisha kuwa choo kinafuata mkondo wa maji.
Ili kupunguza harufu na kuzuia nzi baada ya kutumia choo, nyunyiza jivu, mchanga au chokaa mle ndani.