Je ninawezaje kuzuia matatizo ya kiafya ninapofanya kazi kama mwanamke wa kuosha
Kama itawezekana tumia mpira au gloves kukinga mikono yako.
Hakikisha mikono yako ni kavu. Tumia mafuta au sharubati nzito kutoka kwa mti wa aloe vera baada ya kumaliza kazi yako. Iwapo makucha yako yataharibika jaribu kupaka gentian violet.
Jaribu kuweka bakuli ya kahawa chungu iliyopoa au maji ya vinegar (kikombe kimoja cha vinegar, uchanganye na maji robo kikombe) karibu ya sink. Wakati wowote utakapotumia maji ya sabuni, lowesha mikono yako kwa strungi/ chai ya mkandaa au maji yaliyo na vinegar kwa dakika moja.
Tumia sharubati nzito ya majani yapatikanayo katika eneo uliopo ili kutibu matatizo ya ngozi, vipele, ngozi iliyochomeka au mwasho.
Kusanya kisha osha majani safi halafu yaponde hadi yawe majimaji. Weka mikono yako ndani ya mchanganyiko huo mara kadhaa iwezekanavyo.