Je nini husababisha utasa kwa wanaume

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Sababu za utasa kwa wanaume zinajumuisha:

1. Hatengenezi shahawa za kutosha. Au shahawa zake haziwezi kupiga mbizi na kufikia mishipa ya mwanamke, au haiwezi kuungana na mayai ya mwanamke.

2. Aliugua matumbwitumwi (mumps) akiwa amebaleghe, na ambayo yaliharibu korodani zake. Shahawa zake hazina mbegu.

3. Mbegu zake haziwezi kutoka kwa uume wake kwa sababu ana makovu kwa mishipa yake kutokana na ugonjwa wa zinaa.

4. Ana uvimbe kwa mishipa ya 'scrotum' yake.

5. Anapata shida wakati wa tendo la ngono kwa sababu:

  • uume wake haukui mgumu.
  • uume wake unakuwa mgumu lakini hawezi kutekeleza tendo la ngono.
  • shahawa yake huja mapema sana, kabla hajauingiza uume wake ndani ya sehemu ya uzazi ya mwanamke.

6. Magonjwa kama vile ugonjwa wa kisukari, kifua kikuu na malaria.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011203