Je nini husababisha utasa kwa wanawake

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Sababu za utasa kwa baadhi ya wanawake ni:

Yuko na makovu katika mirija yake au kwa tumbo lake. Makovu haya yanaweza kuzuia yai kupita kwenye mrija, au mbegu kufikia yai. Makovu kwa tumbo pia yanaweza kuzuia yai kujipandikiza tumboni. Wakati mwingine, mwanamke hupata makovu haya lakini hajui kwa sababu haugui. Miaka mingi baadaye, yeye hugundua kuwa ni tasa.

Makovu husababishwa na:

  • maambukizi kutokana na magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa, na huenda hadi kwa tumbo au mirija (pelvic inflammatory disease).
  • kuavyaa mimba ambako sio salama au shida wakati wa kujifungua, ambayo husababishwa na kuharibika au mambukizi kwa tumbo.
  • mazingira chafu wakati aikuwa anawekwa kifaa aina IUD cha kupanga uzazi, ambacho kilisababisha maambukizi.
  • shida baada ya kufanyiwa upasuaji wa sehemu ya uzazi, tumbo, mirija au ovari.

Mwili wake hautengenezi yai. Hii ni kwa sababu labda mwili wake hauna kiwango tosha cha homoni inayohitajika kwa wakati ufaao. Ikiwa hedhi yake huja baada ya siku chini ya 25 au zaidi ya aiku 35, huenda atakuwa na shida ya kutengeneza yai. Wakati mwingine, mwili wake hautengenezi yai ikiwa utapoteza uzani ghafla, au akiwa mnene sana.

Yuko na vimelea tumboni (fibroids). Vimelea hivi vinaweza kuzuia kushika mimba, au kumfanya mwanamke asiweze kubeba mimba.

Magonjwa kama vile virusi vya ukimwi, ugonjwa wa kisukari, kifua kikuu na malaria yanaweza kumfanya mwanamke kuwa tasa.

Njia za kupanga uzazi pia hulaumiwa kwa shida za utasa. Lakini mbinu za kupanga uzazi (isipokuwa sterilisation), hazisababishi utasa, isipokuwa wakati fulani ambapo IUD haijawekwa vizuri na kusababisha maambukizi kwenye tumbo au mirija.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011204