Je nitajuaje ikiwa niko na maziwa ya kutosha na kama maziwa yangu ni mazuri
Wanawake wengi hudhania kwamba hawana maziwa ya kutosha. Hakika, si kweli. Hata akina mama wasiokula chakula cha kutosha kwa jumla huwa na maziwa ya kutosha kwa watoto wao.
Kiwango cha maziwa ambacho matiti hutengeneza (hifadhi yako ya maziwa) hutegemea kiasi ambacho mtoto hunyonya. Jinsi anavyozidi kunyonya, ndivyo maziwa yanavyozidi kutengenezwa. Ukikosa kumpa matiti na badala yake ummpe maziwa kwa chupa, mwili wako utatengeneza maziwa kidogo.
Wakati mwingine yaweza kuonekana kana kwamba mtoto anataka kunyonya kila mara. Ukimpa mtoto maziwa kila anapohisi njaa, maziwa yako yataongezeka. Siku chache zitakazofuata mtoto ataonekana ni kana kwamba ameshiba. Kunyonyesha mtoto usiku kunasaidia kuongeza kiwango cha maziwa ya mama. Jizuie kumuamini yeyote yule - hata mhudumu wa afya - anayekuambia hauna maziwa ya kutosha.
Matiti hayahitaji kuwa makubwa ili kutengeneza maziwa. Mama anavyozidi kunyonyesha watoto zaidi, atahisi matiti yamepungua saizi. Matiti madogo yaweza kutengeneza kiwango sawa cha maziwa yanayotengezwa na matiti makubwa.
Mtoto anapata maziwa ya kutosha iwapo:
Kwa sababu sura ya maziwa ya mama huonekana tofauti na maziwa mengine, wanawake wengine huhofia sio maziwa mazuri. Lakini maziwa ya mama humpa mtoto lishe yote anayohitaji.