Je nitatumia vipi spermicide

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

1. Osha mikono yako ukitumia sabuni na maji.

2. Ili kutumia povu, tikisa chombo cha povu kwa haraka, kama mara 20. Kisha bonyeza mdomo wa chombo hicho kujaza applicator. Ili kutumia jelly au cream, fungilia tube ya spermicide kwenye applicator. Jaza applicator kwa kufinya tube ya spermicide. Ili Kutumia vidonge viingizwavyo kwa uke, ondoa karatasi iliyoifunga na uiloweshe ukitumia maji au uitemee mate. (USIWEKE vidonge hivyo kwa mdomo wako. )

3. Kwa upole weka applicator au kidonge cha uke ndani ya uke wako, mbali nyuma zaidi kitakapo kwenda. 

4. Ikiwa unatumia applicator, finya kutoka juu hadi chini kisha ondoa applicator iliyo tupu.

5. Suuza applicator kwa maji safi na sabuni.

6. Acha spermicide kwa nafasi kwa angalau masaa 6 baada ya ngono. Usiooshe spermicide itoke. Ikiwa utatokwa na cream kutoka kwa uke wako, vaa kisodo, pamba au kitambaa kilicho safi ili kulinda nguo yako.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020417