Je shida gani hujitokeza kwa kula vyakula visivyofaa au chakula kingi
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Wanawake ambao hawapati lishe bora, hasa ikiwa niwanene mno na chakula chao kina wingi wa mafuta au sukari, ni rahisi sana kwao kuugua kutokana na shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo, kiharusi, gallstones, kisukari na baadhi ya saratani. Kuwa mnene sana pia kunaweza kusababisha 'arthritis' kwenye miguu.
Hakikisha kuwa unafanya mazoezi ya kutosha, kula mboga na matunda kwa wingi. Hapa kuna mapendekezo ya kupunguza vyakula visivyofaa:
Epuka vyakula vilivyohifadhiwa ambavyo vina wingi wa mafuta na chumvi, kama vile vibanzi, crisps na soda kama vile Coca Cola.