Je ugonjwa wa kisukari ni nini
Ugonjwa wa kisukari huufanya mwili usitumia sukari iliyoko kwenye chakula vizuri. Ugonjwa huu unaweza kusababisha upofu, kupoteza miguu au mikono, kukosa fahamu na hata kifo. Aina ya 1 ya ugonjwa wa kusikari huanza utotoni. Watu wanaougua Aina ya 1 ya ugonjwa wa kisukari hutumia dawa iitwayo 'insulin' maisha yao yote. Aina ya 1 ya ugonjwa wa kisukari huanza mtu akiwa umri wa miak 40 kwenda juu. Ugonjwa huu ni kawaida kwa watu walionenepa zaidi.
Mwanamke anweza kuugua ugnjwa wa kisukari wakati wa uja uzito. Hii inajulikana kama ujauzito kisukari. Ikiwa wewe ni mja mzito na unahisi kiu kila mara au uzani wako unapungua, muone mhudumu wa afya ili apime kiwango cha sukari kwenye damu yako.
Nini ishara za ugonjwa wa kisukari? Ishara za kwanza:
Baadaye, ishara hatari:
Ishara hizi zote husababishwa na ugonjwa huu. Ili kutambua ikiwa unaugua ugonjwa wa kisukari, muone mhudumu wa afya, au usile kwa muda wa masaa 8, kisha uende kwanye maabara kufanyiwa uchunguzi wa kufunga sukari. Ikiwa viwango vya sukari ni zaidi ya 125 baada ya kuchunguzwa mara mbili, basi unaugua ugonjwa wa kisukari.