Ni jambo muhimu kuoga kila siku kwa kutumia sabuni. Pia:
osha mikono yako kabla ya kula au kutayarisha chakula, baada ya kwenda haja ndogo au haja kubwa, kabla na baada ya kumshughulikia mtoto au mtu anayeugua.
osha sehemu za uzazi kila siku kwa kutumia sabuni na maji. Lakini, usiingize maji ndani ya sehemu za uzazi (kwa wanawake). Sehemu hii hujisafisha yenyewe kwa kutoa majimaji. Ukiosha mle ndani kwa kutumia maji, basi unaondoa kinga ya asili, na hii huenda ikasababisha maambukizi.
hakikisha kuwa unaenda haja ndogo baada ya ngono. Hii husaidia kuzuia maambukizi ya njia ya kupitisha mkojo (lakini haitazuia kushika mimba).
jipanguze vizuri baada ya kwenda haja kubwa. Panguza kuanzia mbele ukienda nyuma. Ukipanguza kutoka nyuma ukija mbele kunaweza kusambaza viini na minyoo kwenye mdomo wa njia ya kupitishia mkojo na sehemu ya uzazi.
Sources
Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.