Je utasa ni nini
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Wanandoa husemekana kuwa tasa ikiwa watashindwa kupata mimba baada ya kushiriki ngono mara kadhaa kwa mwezi kwa muda wa mwaka mmoja, bila kutumia mbinu yoyote ya kupanga uzazi. Wanandoa hawa pia wanaweza kuwa na shida ya utasa ikiwa takribani mimba 3 au zaidi zimeharibika mfululizo.
Mwanaume au mwanamke ambaye tayari ameshapata mtoto pia anaweza kuwa tasa. Anaweza kupatwa na shida kati ya wakati ule alipata mtoto na sasa. Wakati mwingine shida hii haitokani na mwanamke au mwanaume bali ni mchanganyiko wa pande zote mbili. Wakati mwingine wanandoa hawana afya nzuri na hakuna daktari au uchunguzi wowote unaoweza kuonyesha kinachosababisha shida hii.