Jinsi ya kutumia kondomu kwa wanaume

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

1. Ikiwa mwanaume hajatahiriwa, vuta govi nyuma. Finya ncha ya kondomu, na uivalishe kwenye uume uliosisimka.

2. Endelea kuifinya ncha ya kondomu huku ukiivalishe kwenye uume wote. Sehemu ya mwisho itashikilia shahawa ya mwanaume. Ikiwa hutaacha nafasi ya kushikilia shahawa itakapomwagika, basi kondomu inaweza kupasuka.

3. Mwanaume anapaswa kushikilia mdomo wa kondomu baada ya kumwaga shahawa, na aondoe uume wake uliosisimka kutoka kwa uke.

4. Vua kondomu. Usiache shahawa kumwagika au kuvuja.

5. Funga kondomu kisha tupa mbali pale watoto na wanyama hawatafikia.

Mafuta hufanya uke au kondomu kuteleza. Mafuta haya hufanya kondomu zisipasuke na hufanya ngono kuwa salama na kufurahisha zaidi. Mafuta haya lazima yawe na maji, kama vile mate (mate), au K-Y Jelly. Paka mafuta haya katika pande mbili za kondomu iliyovalishwa kwenye uume uliosisimka. Tone la mafuta haya likitiwa ndani ya ncha ya kondomu linaweza pia kumpa mwanaume msisimko zaidi. Usitumie mafuta ya kupikia, mafuta ya mtoto, mafuta ya madini, gel mafuta yenye petroli, mafuta ya ngozi yaliyo na manukato, au siagi. Yanaweza kufanya kondomu kupasuka kwa urahisi.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020411