Jinsi ya kuzuia kifo kutokana na utoaji mimba usio salama

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Wanawake daima hujaribu kutafuta njia za kutoa mimba wakati wakikosa njia mbadala. Kaa mbali na njia zifuatazo. Hizi ni njia hatari sana:

Usiweke vitu vilivyo na ncha kali kama vijiti, waya, au neli plastiki ndani ya uke na tumbo. Hizi zaweza kuharibu tumbo na kusababisha kutokwa na damu hatari kupata maambukizi.

Usiweke mitishamba au mimea katika uke au tumbo lako. Hizi zinaweza kuchoma au kukuwasha vibaya, na kusababisha uharibifu, maambukizi, na kutokwa na damu.

Usiwekee, vitu vya kuchibua kama vile lye, jivu, sabuni, au mafuta ya taa ndani ya uke au tumbo. Pia, usinywe vitu hivyo.

Usichukue dawa au tiba za jadi kwa kiasi kikubwa ili kusababisha uavyaji mimba (aidha kwa mdomo au kuingiza kwa uke). Kwa mfano kunywa dawa ya malaria (chloroquine) au kuacha damu baada ya kujifungua (ergometrine, oxytocin) yaweza kuua wewe kabla ya kusababisha mimba itoke.

Usigonge tumbo lako au kujitupa chini ya ngazi. Hii inaweza kusababisha majeraha na kutokwa na damu ndani ya mwili wako, lakini haiwezi kusababisha mimba kutoka.

MUHIMU: Kamwe usiweke kitu chochote ndani ya tumbo lako au kumruhusu mtu yeyote asiyehitimu kufanya hivyo. Hii inaweza kukuua.

Wachana na njia zisizo salama za kuavyaa mimba. Jaribu kujikinga usipate mimba kabla ya kupata mimba.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020205