Kifua kikuu ni nini

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kifua kikuu husababishwa na viini au Bakteria, viini hivi vinapoingia katika mwili wa mwanamke huwa ameambukizwa kifua kikuu au huishi navyo kwa maisha yake yote.

Walio na afya nzuri wako na uwezo wa kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu na moja kati ya watu kumi huathirika na kifua kikuu maishani mwao.

Lakini mtu asipokuwa na nguvu mwilini kwa sababu ya afya mbaya, akiwa na kisukari, mchanga, mzee, au akiwa ameathirika na virusi vya Ukimwi; Kifua kikuu huanza kuuvamia mwili wake.

Kawaida hii hutokea katika mapafu ambapo vidudu vya kufua kikuu hula na kutoboa toboa mapafu na kuharibu mishipa ya damu. Kadri mwili unapojaribu kuuvamia ugonjwa matundu hujaa usaha na damu.

Matibabu yasipopatikana mwili unaanza kudhoofika kawaida mgonjwa hufa katika muda wa miaka mitano lakini akiwa ameathirika pia na virusi vya ukimwi anaweza kufa baada ya miezi michache asipopata matibabu.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw011604