Kuketi ama kusimama kwa muda mrefu kuna madhara gani kwa afya yangu
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Kama ni lazima uketi ama usimame kwa muda mrefu kazini, unaweza pata madhara ya kiafya. Wakati mwingine, mathara haya yanaweza onekana baada ya miezi ama miaka. Kati ya madhara haya yanaweza zuiwa.
Madhara ya mgongo na shingo: Yanasababishwa na kuketi kwa muda mrefu kama umeinamisha mgongo wako ama kwa kusimama pahali pamoja.
Uvimbe wa mishipa, kufura kwa miguu na kukauka kwa damu kwenye miguu: Unapo simama ama kuketi kwa muda mrefu, ni vigumu kwa damu kutembea kwa urahisi katika miguu yako hasa kama umekunja miguu.