Kwa nini nastahili kujihusisha na Ngono Salama
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Kufanya ngono isiyo salama, au ngono na wapenzi wengi, humweka mwanamke katika hatari ya kupata virusi vya STI na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Maambukizi ya Virusi vya ukimwi yanaweza kusababisha kifo kutokana na UKIMWI.
Magonjwa ya zinaa yasoyotibiwa yanaweza kusababisha utasa, mimba katika mishipa, na kuharibika kwa mimba.
Kuwa na wapenzi wengi pia humweka mwanamke zaidi katika hatari ya kupata magonjwa ya chungu cha uzazi (pelvic inflammatory disease) na saratani.
Wanawake na wanaume wanaweza kusaidia kuzuia matatizo haya yote kwa kujihusisha na ngono salama.