Kwa nini nastahili kujiweka vizuri wakati wa ujauzito na baada ya kuzaa
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Wanawake wengi huona si lazima kutunzwa wakati wa ujauzito wao kwa sababu hawajihisi kama ni wagonjwa. Lakini kuhisi vyema hakumaanishi kuwa hakuna shida. Matatizo mengi ya ujauzito na uzazi kama vile shinikizo la damu au mtoto kukaa vibaya tumboni kwa kawaida huwa haionyeshi dalili zozote zile.
Mwanamke anapaswa kuenda kliniki kabla ya kujifungua mara kwa mara ili wakunga au wahudumu wa afya ambao wamehitimu katika mambo ya kutoa huduma wakati wa ujauzito wanaweza kuchunguza mwili wa mama na kuona kama mimba yake inaendelea vizuri.
Huduma bora za wanawake wajawazito zinaweza kuzuia matatizo kuwa hatari.