Kwa nini niende kwa uchunguzi wa kiafya mara kwa mara

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Magonjwa mengi ya zinaa na saratani hayaonyeshi dalili mpaka ugonjwa unapozidi. mara nyingi ugonjwa unakua umezidi kiasi cha kutotibika.

Ikiwa inawezekana Mwanamke anapaswa kuona Mtaalamu wa afya ili kuangalia mfumo wake wa uzazi kila baada ya miaka mitatu hadi tano, hata kama anajisikia akiwa sawa. Uchunguzi huo ni pamoja na uchunguzi wa fupanyonga, matiti, uchunguzi wa upungufu wa damu, na wa magonjwa ya zinaa kama yuko katika hatari yeyote.

Uchunguzi wa Pap (maelezo zaidi hapo chini) au uchunguzi wa saratani ya mfuko wa uzazi unaweza kufanywa. Hii ni muhimu haswa kwa wanawake wa zaidi ya miaka thelathini na tano 35 kwa sababu wanawake hao wako na uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya mfuko wa uzazi wanapozeeka.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010204