Kwa nini nifikirie hisia za wale nitakao waacha nyuma ikiwa nitahisi kujiua
Jinsi gani familia yako na marafiki watakavyoguswa na habari ya maamuzi yako ya kujiua?Wataathirka kivipi?Kazi, biashara au wateja wangu itakuwa na madhara gani? Kwa nini niwafikirie nitakapofanya uamuzi huo wa kibinafsi wa kujiua?Masawali haya yanaweza kujaa katika akili yako.
Usifanye Kosa. Kujiua kutasababisha madhara makubwa kwa wale walio karibu nawe, na watakaa na madhara hayo maishani mwao.
Kujiua kwako kutasababisha matatizo mengi kwa wale unaowaacha nyuma, haswa familia yako. Mbali na huzuni na mshtuko kwamba watakaopitia, watasumbuliwa na hisia za hatia na aibu maishani mwao. Itawabidi wakabiliane na unyanyapaa wa kijamii au hata kufukuzwa kutoka jamii wanayoishi.
Mbali na matatizo haya, kuna matatizo mengi unayojaribu kuyatoroka unapofikiria kujiua. Masuala haya hayatatoweka unapokufa, bali yatahamia kuwa mzigo wa mtu mwingine, na kusababisha mateso kwa mpendwa wako au mtu wa karibu na wewe,
Hivyo basi fikiria kwa makini kabla ya kufanya uamuzi.