Kwa nini niipange familia yangu

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kila mwaka, wanawake wapatao nusu milioni hufariki kutokana na matatizo ya ujauzito, kujifungua, na utoaji mimba usio salama.

Vifo hivyo vinaweza kuzuiwa kwa kupanga uzazi. Kwa mfano, upangaji uzazi unaweza kuzuia hatari zitokanazo na uja uzito ambazo ni za:

  • Mapema sana. Wanawake chini ya umri wa miaka 18 wako na uwezekano wa kufa wakati wa kujifungua kwa sababu miili yao haijakua kikamilifu. Watoto wao wako na nafasi kubwa ya kufariki katika mwaka wa kwanza.
  • Kuchelewa sana. Wanawake waliokomaa sana hukabiliwa na hatari nyingi wakati wa kujifungua, haswa kama wako na matatizo mengine ya kiafya au wanao watoto wengi.
  • Karibu sana. Mwili wa mwanamke unahitaji muda wa kupona kati ya mimba kadhaa.
  • Wengi sana. Mwanamke aliye na zaidi ya watoto 4 yuko katika hatari kubwa ya kufariki baada ya kujifungua kutokana na kutokwa damu na sababu zinginezo.


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020403