Kwa nini nijilinde baada ya jaribio la kujitoa uhai

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kwa bahati mbaya watu wengi hawana ufahamu kuhusiana na kujitoa uhai, na wanasita kuzungumzia swala hilo. Wengine wanaweza kutojali au kutoa maneno ya kuumiza kimakusudi: kama "Dadako alijiua sababu alikuwa na kichaa". Katika nchi nyingi kuna unyanyapaa unaohusishwa na kujitoa uhai. Ni muhimu kujilinda.

Kuwa mwangalifu nani unayemwambia kuhusu kujitoa uhai. Bila shaka uko na watu wa familia na marafiki unaowaamini na unaweza kuwaeleza wazi kuhusu kujitoa uhai. Lakini ikiwa watu watajua kupitia uvumi kisha wakuulize kuhusu mpendwa wako; ikiwa hutaki kuzungumzia swala hilo, unaweza kusema "Sitaki kuzungumzia swala hilo" au sema jambo linalofuanana na hilo kuwafanya wasikuulize. Usimruhusu mtu yeyote yule anayekulazimisha kuzungumzia jambo ambalo hauhisi sawa kulizungumzia.

Jipe muda wa kupona. Kaa mbali na mtu yeyote yule au jambo linaloweza kukuletea shida. Kaa mbali na watu au sehemu zinazokusumbua. Ikiwa mtu atasema jambo lolote litakalokukera, kaa mbali na yeye haraka iwezekanavyo.

Baadaye, mshtuko ukipungua, na ukijihisi vyema, unaweza kukabiliana na watu wajinga wale hawana hisia na swala la kujitoa uhai. Usifanye hivyo, hadi pale utahisi kuwa uko na nguvu za kiakili na kihisia, na umejikuza kukabiliana na dhiki.


Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020920