Kwa nini nijitahidi katika masomo na mafunzo mazuri
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Masomo yatakupa fahari, mapato bora, na uishi maisha yaliyo na raha na afya. Kwa wasichana wengi, masomo hufungua mlango wa maisha ya baadaye. Hata kama huwezi kuenda shuleni, kuna njia tofauti za kusoma na kuendeleza ujuzi.
Kwa mfano unaweza kusomea nyumbani, kujiunga na kikundi cha mafunzo, au upate ujuzi kutoka kwa mwingine aliye na ujuzi. Unapokuwa na ujuzi mpya, una jambo muhimu la kupa jamaa yako, na unaweza kujikimu pamoja na familia yako.
Kujifunza ujuzi mpya kunaweza kukusaidia kufanya uchaguzi muhimu maishani.