Kwa nini nikague matiti kila mara

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Ni muhimu kwa mwanamke kuchunguza matiti yake kila mwezi, hata baada ya hedhi kukoma kabisa.

Wanawake kadhaa huwa na uvimbe kwenye matiti yao. Uvimbe huu hubadilika kila mara kulingana na siku ya mwezi na hedhi yake. Uvimbe huu huwa laini kabla ya hedhi. Sio kawaida, lakini wakati mwingine uvimbe ambao hauishi mara nyingi huwa ni ishara ya saratani ya matiti.

Mwanamke anaweza kuhisi uvimbe huu mwenyewe, ikiwa atajifunza kukagua matiti yake. Ikiwa atafanya hivi mara moja kwa mwezi, atajielewa zaidi na kuweza kugundua ikiwa kuna jambo ambalo sio sawa.

Ni vigumu kumkagua mwanamke mwenye ulemavu. Hivyo basi, anaweza kukagauliwa na mtu ambaye yeye mwenyewe anamwamini.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010212