Kwa nini nizungumze na mtu ikiwa nitahisi kujiua
Watu ambao hufikiria kujiua haswa wanawake, huhisi upweke, waliotengwa, wanyogovu na walio kata tamaa kwa wakati huo. Hawatamani kuzungumza na mtu yeyote, sababu hufikiria hakuna mtu atakayewasaidia. Sababu inaweza kuwa wanaona haya kuzungumza na mtu jinsi wanavyohisi.
Hata hivyo, kuzungumza na kujadili unavyohisi kutasaidia sana. Unaweza kutafuta mtu unayemuamini ili uzungumze naye(Miongoni mwa marafiki, familia, majirani au wafanyikazi wenza) au labda kuna mhudumu wa afya au kiongozi wa dini katika eneo lako unaweza tafuta msaada. Unaweza pia, kutafuta wanawake wengine wanaopitia shida kama hiyo yako, ambao wako tayari kukusikiza na kujadili mawazo yao na wewe.
Kwa wanawake wengine, ni rahisi kuzungumza na mtu ambaye hawamjui au ambaye hajui shida yao(huona haya kufanya hivyo na pia wanahisi kuwa watapata ushauri ulioa sawa na usio egemea upande mmoja). Katika nchi nyingi na mikoa mingi, kuna nambari ya simu ya kuwasaidia wanaotaka kujinyoga ambayo unaweza kupiga au ukurasa unaoweza kuwasiliana nao katika mtandao, ikiwa utapendelea kuongea na mtu bila kusema jina lako na kwa siri. Hauhitaji kulipia huduma hiyo, na si lazima useme jina lako. Nambari hizo haziegemei upande wowote wa kisiasa na si za kidini na watu wanaofanya kazi hapo hawatakushindilia imani yao kwako. Wako hapo kukusikiza.
Unaweza kuangalia nambari unayoweza kupiga katika nchi yako hapa: http://www.befrienders.org/
Kuzungumza na mtu hakutakusaidia tu kutambua na kuelewa vyema kiini kamili cha shida zako, bali kutakusaidia kupata suluhu zifaazo.
Kuzungumza na mtu ambaye anakujali kunaweza kuwa na mabadiliko. Hata kama utaenda kwa rafiki au jamaa wa familia ambaye utaridhika kukaa naye kunaweza fanya upate mabadiliko makubwa. Kuzungumza kuhusu na kwa nini unavyohisi husaidia pakubwa kupunguza shinikizo hilo, na yaweza kukusaidia uwe sawa katika nafsi yako.