Kwa nini sistahili kutumia mbinu za kutaka kujiua kwa kutuma 'ujumbe' au 'kulipiza kisasi'

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kuwa mwangalifu ikiwa kinachokusukuma kujiuua ni 'kutuma ujumbe' kwa wengine (hii hushuhudiwa sana katika visa vya kujiuua vitekelezwavyo na wanawake) matendo yako yanaweza kuwa yanasukumwa na hasira, wivu, kuumizwa au kisasi, mbali na hamu ya kweli ya kujiua kutokana na msukumo ulionao.


Inaweza kuwa umejaribu mara kadhaa, kutatua migogoro au shida ambazo zinazokusababishia uchungu na mateso, au kubadilisha maisha yako ya taabu. Unaweza kufikiria ya kwamba hakuna mtu karibu na wewe ambaye yuko tayari kukusikiza au kukusaidia. Au labda umeteseka na kisa kilichokufedhehesha (kwa mfano mpenzi wako anayekudanganya, mama mkwe anayekutusi au kukudhalimu wakati wote)Kwa njia yoyote ile, sasa unatafuta njia ya kulipiza kisasi au kuwafanya wateseke.

Unaweza kuwa na mawazo kama: "Mara baada nimejiua/mara baada nimekufa"

  • ... Watajuta kile walichonitendea.
  • ... Hatimaye watasikiza ninachosema na kuona ninamaanisha nini.
  • ... Watagundua kwamba ninahitaji usaidizi na msaada wao mno.
  • ... Watanipenda jinsi ninavyostahili kupendwa.
  • ... Majuto yatawasumbua hadi waniombe msamaha.
  • ... Watabadili mienendo yao.


Kwa bahati mbaya, wakati mwingi (takriban asili mia tisini na tisa nukta tisa sufuri ya muda) wa kinachotarajiwa huwa hakitendeki. Badala yake, ikiwa utaponea kifo utakumbana na ukandamizaji na kashfa za 'kutoheshimu' familia kwa kutaka kujitoa uhai au watafikiria kuwa wewe ni akili tahira/ mwendawazimu. Na ikiwa utafaulu kujinyonga, utakufa na hautaona uzito watu wengine waliokumbana nao. Huwezi furahia kuona huzuni, huruma au mapenzi ya wengine kwako ukifariki.

MUHIMU: USIWAHI kutuma 'jumbe za kujiua' kwa wengine.

Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020913