Kwa nini upangaji uzazi daima uwe chaguo langu
Wanawake wengine hutaka watoto wengi - sanasana katika jamii ambapo watu masikini hunyimwa kipande chao cha haki cha ardhi yao, rasilmali na faida za kijamii. Hii ni kwa sababu, watoto husaidia katika kazi na huwalinda wazazi wao uzeeni. Katika maeneo haya, matajiri pekee ndio hustarehe kuwa na watoto wachache wanaoweza kuwalea.
Wanawake wengine wangelipenda kudhibiti kiwango cha watoto walionao. Hii hufanyika wakati wanawake wana fursa ya kusoma na kupata mapato, na pale ambapo wanaweza kujadiliana na wanaume kwa njia sawa zaidi.
Haijalishi pale ambapo mwanamke anaishi, atakuwa na afya zaidi kama anaweza kudhibiti idadi ya watoto anaowapata na wakati atakao wapata. Bado - kuamua kutumia - au kutotumia - upangaji uzazi daima kunapaswa kuwe chaguo la mwanamke. Uko na haki ya kufanya uamuzi unaofaa kuhusu upangaji uzazi.