Kwa nini vurugu na ukatili dhidi ya wanawake ni tatizo
Kila siku, wanawake wanapigwa makofi, mateke, kupigwa, unyonge, kutishiwa maisha, kudhulumiwa kingono au kimapenzi, na hata kuuwawa na wapenzi wao. Lakini mara nyingi hatuwezi kusikia kuhusu vurugu hii, kwa sababu wanawake wanaonyanyaswa huwa wanaskia aibu, upweke, na wana hofu ya kuongea dhidi ya huu ukatili. Madaktari wengi, wauguzi, na wafanyakazi wa afya hawatambui vurugu kama tatizo kubwa la kiafya.
Sura hii inahusu aina mbalimbali za vurugu kutokea kwa wanawake na wasichana. Na inaweza kukusaidia kuelewa ni kwa nini vurugu hutokea, nini unaweza kufanya kuhusu vurugu, na jinsi gani unaweza kufanya kazi kwa ajili ya mabadiliko katika jamii yako.
Ingawa hii sura inaongea kuhusu vurugu kati ya mwanamke na mwanaume, vurugu inaweza kutokea katika uhusiano wowote wa karibu: kwa mfano, kati ya mama mkwe na mke wa mwanawe mpya, kati ya wazazi na watoto wao, kati ya watoto wakubwa na wadogo, kati ya wanafamilia na mtu mzee ambaye anaisha katika nyumba moja, na kati ya washirika wa jinsia moja.