Kwa nini wanawake hukaa na wanaume wanaowadhuru

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

"Kwa nini yeye hukaa?" Ni swali la kwanza watu wengi huuliza wanaposikia kuhusu mwanamke anayenyanyaswa. Kuna sababu nyingi kwa nini mwanamke anaweza huchagua kukaa katika uhusiano wa dhuluma. Sababu zenyewe ni:
  • Hofu na vitisho: Mwanamume anaweza kuwa amemwambia, "Nitakuua, niwaue watoto, nimuue mama yako. . . ikiwa utajaribu kuondoka. " Anaweza kufikiria kwamba anafanya kila awezalo ili kujilinda na kuwalinda wengine kwa kukaa.
  • Kukosa pesa/fedha, na mahali pa kwenda: Hii ni kweli haswa ikiwa mwanamume yuko na mamlaka na pesa zote na hajamruhusu mkewe kuona familia yake na marafiki.
  • Kukosa ulinzi: Anaweza kosa kizuizi cha kumzuia kumfuata mkewe na kumuua.
  • Aibu: Mwanamke anaweza kuhisi kwamba kwa namna fulani ni kosa lake, au kwamba yeye anastahili.
  • Imani za kidini au za kitamaduni: Mwanamke anaweza hisi kwamba ni wajibu wake wa kutunza ndoa, bila kujali atagharamika kivipi.
  • Matumaini ya mabadiliko: Anaweza kuhisi bado anampenda mumewe na anataka uhusiano wao uendelee. Anaweza kufikiria kuwa kuna njia ya kusimamisha vurugu.
  • Hukumu ya kuacha watoto bila baba.

Lakini labda swali bora la kuuliza ni, "Kwa nini mwanamume haendi?" Ikiwa tutauliza kwa nini mwanamke haendi, inaonyesha ya kwamba tunafikiria kuwa ni tatizo la mwanamke binafsi kutatua. Ni makosa kufikiria vurugu ni tatizo lake tu.

Jamii nzima inahitajika kuwajibika kwa afya na ustawi wa kila mtu katika jamii hiyo.

Ni mwanamume anayefanya uhalifu kwa kukiuka haki ya mwanamke ya kuishi huru mbali na madhara ya kimwili, au kwa kumuua. Matendo yake yanapaswa kushurutishwa na kusimamishwa.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020114