Kwa nini wanawake walio na ulemavu mara nyingi wanakabiliwa na matatizo ya ngozi
From Audiopedia - Accessible Learning for All
Kama wewe hukaa au kulala mara nyingi unaweza ukapata na shinikizo la vidonda. Maumivu haya huanza wakati ngozi ya sehemu ngumu ya mwili inapobanwa dhidi ya kiti au kitanda mishipa ya damu hubanwa ikafungika, ili kwamba ngozi haipati damu ya kutosha.
Ikiwa muda mwingi utapita bila ya kusonga, baka nyeusi au nyekundu litaonekana kwenye ngozi. Iwapo shinikizo litaendelea kidonda kitaanza kuchipuka na kupenya mwilini.
Au vidonda vinaweza kuanza ndani kwenye mifupa na kuenea hatua kwa hatua hadi nje ya ngozi. Bila matibabu, ngozi yaweza kuharibika.