Kwa nini wanawake walioolewa hutamani kujitia kitanzi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Katika nchi nyingi zinazoendelea, ndoa ni chanzo kubwa ya mawazo kwa wanawake. Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusababisha tabia ya kujiua ni:

  • Ndoa za umri mdogo (wakati mwingine umri ni mdogo).
  • Ukosefu wa uhuru wa kuchagua mpenzi wao (Ndoa za kupangwa).
  • Migogoro ya mahari.
  • Kushinikizwa kupata watoto mapema katika ndoa (katika visa vingi wapate mtoto wa kiume)
  • Mume kutegemewa kwa maswala ya kiuchumi au mfumo wa familia ya pamoja.
  • Masuala ya fedha.
  • Unyanyasaji wa nyumbani.
  • Migogoro ya kifamilia au mizozano.
  • Ukosefu wa udhibiti na mamlaka kwa maisha ya mtu binafsi kwa ujumla.
  • Ukosefu wa haki sawa.

Bi harusi vijana mara nyingi huondolewa kwa wenzao na wazazi wao, waendapo kuishi na bwana harusi baada ya kuolewa. Matokeo yake yakiwa ni, kupoteza usaidizi kutoka kwa familia yao na marafiki. Wanakabiliwa mapema na tendo la kujamiiana kusikohitajika, na ujana wao kuharibiwa na mazingira magumu na kuhusishwa na vurugu kutoka kwa washirika wao kuliko wengine wanaoa baadaye. Yote haya huwaweka katika hatari kubwa ya kujiua.


Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020904