Nchi nyingi zimeshuhudia kuongezeka kwa kasi kwa visa vya kujiua kwa watu wazima wazee(walio na umri zaidi ya miaka 65).
Sababu zinazokisiwa ni:
Maadili ya jadi na desturi kuvurugika kwa haraka katika nchi nyingi (kutokana na maisha ya kisasa ). Badala ya kuwaheshimu na kuwathamini wazee, baadhi ya jamii huanza kuwaangalia wazee hao kama mizigo isiyokuwa na maana. Kuwatunza inakuwa kazi ya shida au inayowachosha. Katika kutafakari kutokuheshimwa huku, wazee wengi hujiua kwa sababu hawataki kuwa mzigo tena kwa familia zao na jamii.
Uhamiaji wa lazima kwa wapendwa wao. Katika nchi nyingi, siku hizi, watoto na wajukuu hulazimika kuhama kwa sababu hakuna chakula au kazi nyumbani, au kwa sababu viwanda hutoa fedha zaidi Jijini. Baadhi yao huhama maili/masafa marefu kuishi karibu na kazi. Wakati huu wa ' uhamiaji ', wazazi wao na babu huachwa pekee yao bila mtu wa kuwatunza. Wengine wao huhisi upweke, wanyonge na wenye huzuni kwamba wao hupendelea kujiua.
Wanawake mara nyingi hufikiria uzee ni " msimu wa hasara ". Wanapaswa kuomboleza vifo vya marafiki wengi na wapendwa. Hasara ya waume wao husababisha huzuni kubwa kwa wanawake wajane na kwa wakati uo huo wao hupatikana katika hali ngumu ya kiuchumi. Wale ambao hawapati msaada wa kutosha kutoka kwa marafiki na familia, mara nyingi hushindwa kukabiliana na matatizo haya.
Kutojiamini na swala la kustaafu. Hii hali haswa inashuhudiwa katika nchi zilizoendelea, ambapo wanawake wengi hujisaidia wenyewe huko. Muda unavyoyoyoma wanawake wazee hujikuta wamefika mwisho wa kufanya kazi/ajira, kustaafu kwao hufanya wakose kujiamini na kujitegemea. Hujiona hawana maana na wasiohitajika. Kupoteza mawasiliano ya kijamii yanayohusiana na kazi huwafanya kuhisi upweke na kutelekezwa.
Masuala ya afya. Kutokuwa na afya njema kutokana na ugonjwa sugu na / au maumivu, mara nyingi husababisha kuishiwa na nguvu ya kutembea/kuzunguka, uhuru wa kibinafsi na utu ni baadhi ya sababu zinazowafanya wanawake wazee kutotaka kuishi tena.