Kwa nini wasichana wadogo hutamani kujiua

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Wasichana wanaofikisha umri wa kubalehe hupata changamoto na shida, haswa katika nchi zinazoendelea.

  • Wakati mwingi, huondolewa shuleni na kulazimishwa kuwajibika na masuala ya nyumbani. Hawapewi nafasi ya kufanya maamuzi, ila kusahau uwezo na matarajio walio nayo.
  • Hawaruhusiwi kujumuika na watu wengine wa nje.
  • Wakati mwingine hawaruhusiwi kutoka nyumbani mwao.
  • Wakati mwingine hulazimishwa kuanza maisha ya ndoa.
  • Hawashauriwi au kufunzwa vyema kuhusu maisha ya ngono kabla ya ndoa, na mara nyingi hudhulumiwa. Kisha wasichana hawa hupata mimba za mapema na kulazimika kukumbana na masengenyo na uonevu kutoka kwa wanarika na jamii ikibainika wazi kwao.

Wasichana wengi na wanawake vijana hukosa raha, huku wakikabiliana na shinikizo kutoka kwa (wanarika, familia, mtandao wa kijamii au sinema)wanaotarajia wakae na kuwa na vitendo aina fulani (kulingana na dhana ya urembo ulio bora). Wao huhisi hawavutii na hawastahili kupendwa na kukubaliwa. Hisia hizi zinaweza kuwafanya wajidhuru kama kujikata au kujihusisha na madawa ya kulevya.


Sources
  • Felicitas Heyne, Psychologist
  • Audiopedia ID: sw020905