Kwa nini watu wanatumia vibaya madawa na pombe
Watu wengi huishia kutumia vibaya madawa ya kulevya na pombe ili kuepuka matatizo katika maisha yao. Aina yote ya watu hufanya hivyo. Lakini watu ambao wazazi wao walitumia vibaya pombe au madawa wana uwezo mkubwa zaidi kujaribu na kutatua matatizo yao kwa njia kama hiyo ya wazazi wao. Hii ni kwa sababu 'udhaifu' wa matumizi mabaya ya pombe au mihadarati yaaweza kupitishwa kutoka kwa wazazi hadi kwa watoto. Na watoto wanapowaona wazazi wao wakitumia pombe au madawa ya kulevya kutatua shida zao nao hujifunza tabia io hiyo.
Pombe na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya pia ni ya kawaida miongoni mwa watu ambao hawananmatumaini yoyote ya kubadili mienendo yao ya maisha. Wakimbizi au au wanaokabiliwa na changamoto kadhaa kama - kupoteza kazi au njia ya kujikimu maishani, kufiliwa au kuwadhwa na mpenziwe - wako katika hatar kubwa ya kutumia mihadarati na vileo. Wanawake mara nyingi hujihusisha na utumizi mbaya wa mihadarati kwa sababu hawahisi ikiwa wako na uwezo - au nguvu kubadili mienendo yao. Huenda wakahisi wanategemea mpenzi wao. Na kama wanawake wako na hadhi ya chini katika jamii, inaweza kuwa vigumu kwao kujithamini. Mihadarati na pombe kwa kawaida hufanya matatizo yote haya yote kuwa mabaya zaidi, na watu hujusikia hawana uwezo wa kuboresha maisha yao. Badala ya kutafuta njia za kuboresha hali zao, watu wengi ambao wanatumia vibaya madawa ya kulevya au pombe hutumia muda wao, pesa, na afya kwa kujaribu kuepuka na kusahau matatizo yao.
Wakati mtu anapojihusisha na mihadarati au pombe, akili na mwili unaweza kuanza kuhisi haja ya madawa ya kulevya. Wakati akili inahisi haja hii, ni wito tegemezi. Wakati mwili wa mtu unahisi haja ya kutumia mihadarati na anaweza kuwa mgonjwa ikiwa hatatumia madawa hayo. Pombe na baadhi ya dawa inaweza kusababisha kutegemea madawa ya kulevya. Wakati mtu atategemea mihadarati, atahitaji mihadarati au pombe zaidi ndio ahisi matokeo yake.