Madhara yapi ya kawaida ya mchanganyiko wa vidonge

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kutokwa na damu kusikofuata mzunguko wake au spotting (kutokwa na damu wakati mwingine kuliko kutokwa na damu yako ya kawaida ya kila mwezi). Mchanganyiko wa vidonge hufanya siku zako za hedhi kuwa kidogo na damu kuwa nyepesi. Hii ni mojawapo ya madhara yanayoshuhudiwa unapochanganya vidonge vya upangaji uzazi. Kupunguza spotting, kuwa makini kumeza kidonge wakati uo huo kila siku. Ikiwa spotting itaendelea, pata ushauri wa mhudumu wa afya ili kuona ikiwa kubadilisha dozi ya projestini au estrogen itasaidia. Ikiwa damu yako ya kila mwezi haiji katika muda wa kawaida na umekosa baadhi ya vidonge, endelea kumeza dawa yako lakini muone mhudumu wa afya ili kujua ikiwa wewe ni mjamzito.

Kichefuchefu, hisia ya kutaka kutapika, kwa kawaida hupotea baada ya mwezi 1 au miezi 2. Ikiwa kinakusumbua, jaribu kumeza dawa na chakula au wakati mwingine wa siku. Wanawake wengine hupendelea kumeza kidonge kabla tu ya kwenda kulala usiku kwani huwasaidia.

Maumivu makali ya kichwa katika miezi michache ya kwanza ni ya kawaida. Dawa ya kutibu maumivu makali ya kichwa husaidia. Ikiwa utaumwa na kichwa zaidi au upate kizunguzungu, hii inaweza kuwa dalili/ishara.

Ikiwa unasumbuliwa na mabadiliko yoyote ya mwili baada ya kuanza kutumia vidonge vya upangaji uzazi, zungumza na mhudumu wa afya. Anaweza kupendekeza kidonge tofauti.

Ikiwa umepewa dawa mpya wakati unatumia kidonge, muulize mhudumu wako wa afya kama unapaswa kutumia mbinu ya kuzuia au kutoshiriki ngono wakati unapotumia dawa. Baadhi antibiotics na dawa nyinginezo husababisha vidonge kutofanya kazi vyema.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw020424