Magonjwa ya zinaa ni nini

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Magonjwa ya zinaa ni maambukizi kutoka kwa mtu moja hadi mwingine wakati wa kujamiiana au ngono. Aina yoyote ya kujamiiana yaweza kusabisha maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Yaweza kuwa kujamiiana kwa kawaida pale ambapo uume unapoingizwa ndani uke, au umme unapoingizwa kwa tundu la haja kubwa, au uume unapoingizwa kwa mdomo (mdomo kwa umme, mdomo kwa uke). 

Wakati mwingine maambukizi ya zinaa hutokea wakati wa kusugua na kugizishana uume au uke uliyoambukizwa. Magonjwa ya zinaa yanaweza kuambukizwa kutoka kwa mama mjamzito hadi kwa mtoto ambaye bado hajazaliwa au wakati wa kuzaa. Magonjwa ya zinaa huongeza maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Iwapo itatibiwa mapema, magonjwa ya zinaa yanaweza kusababisha:

  • Gumba na Utasa kwa mwanamume na mwanamke.
  • Watoto kuzaliwa kabla ya wakati, ama mtoto mwenye udhaifu, kipofu, mgonjwa au aliyefariki
  • Mimba isiyokuwa sawa (iliyoko nje ya nyumba la uzazi)
  • Kifo kutokana na maambukizi
  • Maamivu makali chini ya kitovu (tumbo la chini)
  • Saratani ya mfuko wa uzazi.

Matibabu ya mapema ya magonjwa ya zinaa kwa wapenzi yaweza kuzuia shida.

Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010502