Magonjwa ya zinaa ya kawaida ni yapi

From Audiopedia - Accessible Learning for All
Jump to: navigation, search

Kutokwa usiokuwa wa kawaida: Mabadiliko katika viwango, rangi au harufu ya kutokwa huku kwenye sehemu yako ya uzazi humaanisha kuwa una maambukizi, lakini ni vigumu kutambua kutokana na kutokwa huku ni maambukizi gani uliyo nayo.

Trichomonas: Ugonjwa huu wa zinaa husababisha kutokwa ambako kuna harufu mbaya, mwasho mwekundu katika sehemu ya uzazi, uchungu au kuhisi i kama unachomeka unapoenda haja ndogo. Wanaume huwa hawana ishara zozote, lakini wanaweza kubeba viini kwenye uume wao na kumwambukiza mwanamke wakati wa ngono.

Upele na Chawa: Kujikuna kwenye nywele za sehemu ya uzazi au karibu na sehemu hizi husababishwa na upele na chawa.

Kisonono na chlamydia: Magonjwa haya ya zinaa ni hatari sana, lakini rahisi kutibu ikiwa yatagunduliwa mapema. Yasipotibiwa kwa wakati, yanaweza kusababisha maambukizi zaidi na utasa katika wanawake na wanaume.

Vimelea kwenye sehemu za uzazi: Vimele hivi husababishwa na virusi. Vimelea kwenye sehemu za uzazi huonekana kama vimelea kwenye sehemu nyingine ya mwili. Kuna uwezekano kuwa una vimelea lakini usijue, hasa vikiwa ndani ya sehemu ya uzazi.

Vidonda kwenye sehemu za uzazi: Vidonda vingi vinavyopatikana kwenye sehemu za uzazi husambazwa kwa njia ya ngono. Nivigumu kutambua ni ugonjwa upi unasababisha vidonda hivi, kwa sababu vidonda vinavyosababishwa na kaswende na chancroid hufanana.

Kaswende: Ugonjwa huu wa zinaa ni hatari sana, na madhara yake huenea mwilini na huweza kukaa mwilini kwa miaka kadhaa. Husababishwa na bakteria na unaweza kutibiwa ikiwa utagunduliwa mapema. Bila matibabu, kaswende inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, kupooza, ugonjwa wa kiakili au hata kifo.

Chancroid: Ugonjwa huu wa zinaa husababishwa na bakteria. Unaweza kusababisha kidonda kimoja au zaidi kwenye sehemu ya uzazi au sehemu ya kutoa haja kubwa. Kidonda hiki huvuja damu kwa urahisi, kufura kwa mishipa ambayo iko kwenye sehemu za uzazi, na joto mwilini.

Malengelenge ya sehemu za siri (genital herpes): Ugonjwa huu wa zinaa husababishwa na virusi. Husababisha vidonda kwenye sehemu za uzazi au kwenye mdomo, ambvyo huja na kwenda kwa miezi au miaka kadhaa. Utahisi kuwashwa, au kujikunakuna kwenye sehemu ya uzazi au kwenye mapaja, na kupata vidonda vidogovidogo ambavyo hupasuka na kugeuka kuwa vidonda vikubwa.

HIV: HIV, virusi vinavyosababisha UKIMWI, husambazwa sana wakati wa ngono ambayo sio salama. Husambazwa wakati shahawa, majimaji kutoka kwenye uuke, au damu ya mtu aliyeambukizwa na virusi vya HIV ikiingia mwili wa mtu mwingine. Vidnda kwenye sehemu za uzazi hurahisisha usambazaji wa virusi hivi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Shahawa na kutokwa kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa wa zinaa au virusi vya HIV kuna kiwango kikubwa cha virusi vya HIV. Wanawake wanaweza kuambukizwa virusi vya HIV kwa urahisi kuliko wanaume wakati wa ngono. Unaweza kuambukizwa virusi vya HIV na mtu anayeonekana kuwa mwenye afya.

Hepatitis B (Macho ya Njano): Maambukizi haya ni atari sana na husababishwa na virusi ambavyo huathiri maini. Husambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, hasa wakati wa ngono. Unaweza kusababisha ishara kama vile joto mwilini, kukosa hamu ya kula, uchovu, macho na/au ngozi ya njano, maumivu tumboni, mikojo mizito na haja nyeupe.

Unapotibu magonjwa ya zinaa:

  • hakikisha kuwa mpenzi wako pia anatibiwa.
  • meza dawa zote
  • acha kushiriki ngono au tumia kondomu wakati wa ngono hadi ishara zote zimetokomea NA wewe na mpenzi wako mmemaliza dawa.
  • muone mhudumu wa afya ikiwa haupati nafuu baada ya kutumia dawa.
  • shiriki ngono iliyo salama


Sources
  • Burns, A. A., Niemann, S., Lovich, R., Maxwell, J., & Shapiro, K. (2014). Where women have no doctor: A health guide for women. Hesperian Foundation.
  • Audiopedia ID: sw010505